HAYA HAPA MAELEZO JUU YA ASILIMIA ZA MKOPO MWANAFUNZI ALIOUPATA KUTOKA HESLB

Campus Admin 2018-10-18 05:33:42 Notice Board

Wanafunzi wengi wamekuwa wakihangaika kupata uhakika wa asilimia za mkopo walizo zipata kwa wale waliofanikiwa kupata mkopo kwa awamu ya kwanza. Ufafanuzi ni kwamba asilimia za mkopo huwa kwenye michanganuo ya ada tu na si fedha ya kujikimu. Hivyo basi asiimia za kiasi cha fedha mwanafunzi atakazolipiwa ada na bodi ya mikopo ya elimu ya juu zitawekwa kwenye account zao walizoombea mikopo zikionyesha kila mchanganuo wa fedha watakazonufaika. Lakini pia mchanganuo huo utapatikana kwenye mbao zao za matangazo, vyuoni kwao walikochaguliwa. Hivyo wanatakiwa kuwa na subira kidogo huku mchakato huo ukifuatwa.