SERIKALI YA SINGAPORE YAFUTA MFUMO WA MADARAJA (DIVISION) YASISITIZA ELIMU SIO MASHINDANO.

Campus Admin 2018-10-10 04:31:00 Current affair

Mfumo wa madaraja (Division) ni moja ya mfumo wa muda mrefu sana wa upangaji wa matokeo ya kitaaluma kwa wanafunzi wa ngazi mbalimbali katika mataifa mengi ikiwemo Tanzania. Hali imekuwa tofauti kwa nchi ya Singapore ambapo mfumo huo umeondolewa rasmi na waziri wa elimu Bwana Ong Ye Chong. Waziri huyo amesema kuwa "iwe mwanafunzi amemaliza wa kwanza au wa mwisho mfumo huu wa ukokotoaji matokeo hautotumika tena nchini Singapore kuanzia mwaka ujao" waziri huyo anatumaini kuwa hatua hiyo itawaonesha wanafunzi kuwa "Kujifunza si mashindano bali ni hiari na utayari wa mtu binafsi" Kuanzia mwakani vitabu vya ripoti ya mwanafunzi havitaonesha nafasi ya mwanafunzi darasani bali itaonesha taarifa kama Wastani wa ufaulu wa wanafunzi wote darasani, alama ya juu sana na ya chini sana darasani,wastani wa ufaulu wa somo husika na aidha kufaulu au kufeli kwa matokeo ya mwisho wa mwaka. Waziri wa elimu Bw.Ong amesema kuwa lengo ni ni kumwezesha kila mwanafunzi kujikita katika maendeleo yake binafsi katika ujifunzaji na kuondoa hali ya kushindana na wengine. Anatanabaisha kuwa hata mitihani ya kuvuka chekechea na darasa la kwanza nayo itaondolewa na watavuka hatua moja kwenda nyingine kwa kuzingatia ubora wa mwanafunzi mwenyewe katika ujifunzaji wao, Walimu wataendelea kupata taarifa za maendeleo ya wanafunzi wao kama kawaida kupitia majadiliano, mazoezi, kazi za vikundi, kazi za nyumbani (homework) na maswali ya ana kwa ana lakini watatumia ubora na ufanisi wa mwanafunzi mwenyewe katika kuvuka madaraja hayo (chekechea na darasa la kwanza) na si alama zake (Grades) hii ina maana kuwa kama hukujifunza kwa bidii inakuwa ngumu kuvuka hatua moja kwenda nyingine aidha wazazi watapokea taarifa za maendeleo ya wanafunzi kupitia vikao vya wazazi. Waziri huyo ameingeza kuwa "hatua hii imelenga kuwajengea wafunzi tabia ya kujifunza zaidi na sio kutafuta matokeo ya juu katika mitihani.".