TAHLISO YAWATAKA WANAFUNZI WANAOSUBIRI MIKOPO KUWA NA SUBIRA

Campus Admin 2018-10-30 01:01:30 Campus News

Kamishina idara ya Mikopo na udahili TAHLISO, ndugu Lecton Moris, amewataka wanafunzi ambao bado hawajapata mkopo kutoka bodi ya mikopo wawe na subira kwani bado kunaidadi ya wanafunzi wako katika orodha ya wanufaika isipokuwa bado tu majina yao kutolewa. Lakini pia kwa watakaokosa hata kwenye hiyo orodha amewaasa kuwa watulivu maana kunanafasi ya kukata rufaa. Kuna wanafunzi wananipigia simu wakilalamika kuwa wamekosa Mikopo ,naomba niwashauri kuwa wawe wavumilvu kidogo kwani bado majina takribani 12000 yanakuja bila kusahau nafasi ya kukata rufaa hivyo naomba tusubiri kwani mchakato unaendelea na hatuwezi kuingilia zoezi katikati alitaarifu Lecton Pia alieleza kuwa TAHLISO ipo kuwasemea wanafunzi wenye mahitaji makubwa zaidi katika mkopo huu wakiwemo yatima na walemavu na hivyo wtafanya hivyo kadri wawezavyo ili kuwatatulia changamoto zinazoweza kukwamisha malengo yao ya kimasomo. Ikumbukwe tu kuwa kunaidadia kubwa ya wanafunzi ambao bado matumaini yao ya kusoma yanategemea na msaada wa serikali kupitia ufadhiri wa mikopo inayotolewa na bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu nchink, hivyo kutokuona majina yao katika orodha ya awamu ya kwanza na ya pili, kunazua wasiwasi kubwa kwao.