USAMBAZAJI WA PICHA ZA NGONO NA PONOGRAFIA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII

Campus Admin 2018-10-30 04:53:13 Current affair

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) inaukumbusha umma juu ya umuhimu wa matumizi sahihi na salama ya huduma ya mawasiliano pamoja na mitandao ya kijamii. Hivi karibuni kumekua na tabia chafu kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii wakiongozwa na wasanii wa filamu na muziki nchini jutengeneza na kusambaza picha,sauti na maandishi ya ngoni,au yenye muelekeo wa kingono katika mitandao ya kijamii. Ikumbukwe kwamba, kuchapisha,kusambaza au kusababisha kusambaza picha,maandishi,vibonzo vya ponografia au ponografia yoyote iliyo ya kiasherati au chafu katika mitandao ya kijamii,tovuti au mfumo wa kompyuta *ni kosa la jinai* kwq mujibu wa sheria ya kanuni ya adhabu (penal code) sura ya 16 ya sheria za jamhuhuri ya muungano wa Tanzania,sheria ya makosa ya mitandao ya mwaka 2015 na kanuni na maudhui ya mwaka 2018. Aidha TCRA inarudua tena kutoa onyo kwa wale wote wenye tabia ya kusambaza (forwqrd) jumbe,picha,sauti,katuni au maandishi ya ngono,ponographia na yasiyo ya kimaadili katika mitandao ya kijamii hasa Facebook,Twitter,instagram na makundi ya whatsApp. Tayari hatua kali za kisheria zimechukuliwa kwa wahusika wote na zinaendelea kuchukuliwa dhidi ya mtu yeyote atakaebainika kujihusisha na utengenezaji,usambazaji wa picha,sauti,vibonzo au maandishi ya ngono,yenye muelekeo wa ngono yasiyo na maadili . TCRA inapenda kuhimiza jamii kutumia huduma za mawasiliano na fursa zake kwa namna isiyovunja sheria,matunizi ya mitandao ya kijamii yawe sahihi,salama na kwa ajili ya maendeleo. IMETOLEWA NA: MKURUGENZI MKUU TCRA