RAIS WA LIBERIA AFUTA ADA KWA VYUO VIKUU VYOTE VYA UMMA

Campus Admin 2018-10-25 04:41:04 Education

Rais George Weah wa Liberia jana ametangaza kufuta ada kwa vyuo vikuu vyote vya umma nchini humo kwa wanafunzi wa shahada ya kwanza (undergraduate). Pia ameeleza kuwa serikali yake inapanga kutoa ruzuku kwa vyuo vikuu binafsi ili kuvipa unafuu viweze kupunguza ada kwa wanafunzi wanaosoma vyuo hivyo. Liberia ina vyuo vikuu 9 vya umma na 10 vya binafsi ambavyo vingi vinamilikiwa na mashirika ya dini. Liberia imekuwa nchi ya kwanza barani Afrika kufuta kabisa ada kwa wanafunzi elimu ya juu, licha ya kupigana vita ya wenyewe kwa wenyewe kwa karibu miaka 20 iliyoharibu kabisa uchumi wa nchi hiyo. Rais Ellen Johnson Sirleaf aliyeingia madarakani mwaka 2006 alianza kuusuka upya uchumi wa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika inayotegemea madini, uvuvi na mazao ya misitu kuendesha uchumi wake. Kwa kipindi cha miaka michache tangu kukoma kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchi hiyo imepiga hatua kubwa kimaendeleo na kuzizidi nchi nyingi zilizokuwa na amani ikiwemo Tanzania. Mwaka 1990 wakati nchi hiyo ikiwa katika vita, shilingi moja ya Tanzania ilikua sawa na dola 65 za Liberia. Lakini kwa sasa Dola 1 ya Liberia ni sawa na shilingi 14.6 za Tanzania. That means sarafu yao imezidi kuimarika siku hadi siku na yetu ikizidi kuporomoka mara dufu. Rais Weah ametoa rai kwa nchi nyingine za Afrika kufuta ada kwa vyuo vikuu vya umma na kutoa ruzuku kwa vyuo vikuu binafsi ili kupunguza gharama ya elimu. Amesema wanafunzi wengi barani Afrika hupoteza fursa ya kusoma elimu ya juu kutokana na kukosa uwezo wa kulipa ada. Hivyo basi katika karne hii ambapo bara la Afrika linahitaji sana wataalamu mbalimbali, gharama za elimu hazipaswi kuwa kizuizi cha mtu kusoma.!