RITA yasisitiza wanafunzi kufanya uhakiki wa vyeti vya kuzaliwa na vifo

Campus Admin 2019-05-14 11:09:55 Campus News

WAKALA wa Usajili na Udhamini (Rita) imetaja masharti ya uwasilishaji wa nakala ya vyeti vya kuzaliwa na vifo kwa waombaji wa mikopo ya wanafunzi wa vyuo vikuu Ilielezwa kuwa baada ya uhakiki cheti kilichohakikiwa kitatumwa kupitia anuani ya mwombaji katika mtandao. Pia, ilielezwa kila mwombaji anatakiwa awasilishe kivuli cha cheti kinachosomeka kwa ajili ya uhakiki huo ikiambatanishwa na nakala ya risiti ya malipo. Aidha,ilielezwa kuwa utaratibu uliotumika katika kuhakiki vyeti vya kuzaliwa ndiyo utakaotumika kuhakiki vyeti vya kifo vya wazazi. Hii ni maalum na muhimu sana kwa wahitimuwa kidato cha sita wanaotarajiwa kujiunga na vyuo vya elimu ya juu. Unaweza tumia link hii kufanya uhakiki wa vyeti mapema ili kuepuka chagamoto wakati wa uombaji wa mikopo tumia http://uhakiki.rita.go.tz/uhakiki/ kufanya uhakiki wa vyeti vyako