Mkapa aula tena UDOM

Campus Admin 2019-05-14 20:26:50 Campus News

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amewateua Rais mstaafu Benjamin Mkapa na Profesa Ignas Rubaratuka kuendelea na nyadhifa zao kwa mara nyingine. Rais mstaafu Mkapa anaendelea na wadhifa wake wa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), kwa kipindi cha pili mfululizo. Wakati Profesa Rutaratuka anaendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa kipindi cha pili. Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa leo Jumanne Mei 14, 2019 imebainisha kuwa uteuzi huo umeanza tangu Mei 10 mwaka huu.