Darasa la saba waitwa kujiunga JKT

Campus Admin 2019-06-11 17:20:41 Campus News

VIJANA waliomaliza elimu ya darasa la saba wenye umri wa kuanzia miaka 16 hadi 18 wenye ndoto za kupata mafunzo ya jeshi sasa wamealikwa kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa kujitolea.\r\n\r\nMiongoni mwa sifa zinawaruhusu vijana hao kujiunga na jeshi hilo ni pamoja na kutokuwa na alama ya mchoro wowote ikiwamo tatoo mwilini, asiwe amejihusisha na matumizi ya dawa za kulevya ikiwamo bangi.\r\n\r\nKwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano Makao Makuu ya JKT mlango huo umefunguliwa na Mkuu wa Jeshi hilo na vijana hao watajiunga na waliohitimu kidato cha nne.\r\n\r\nMwaliko huo unawahusu pia wale wenye vipaji vya michezo mbalimbali na sanaa waliomaliza darasa la saba au kidato cha nne.\r\n\r\nKatika taarifa hiyo vijana hao wanatakiwa kuomba na hatimaye kuchaguliwa kujiunga na mafunzo hayo kupitia ofisi za wakuu wa mikoa na wilaya wanazoishi.\r\n\r\nImeelezwa kuwa hatua ya kuchagua vijana hao inaanza Juni 2019, hivyo vijana watakaochaguliwa watatakiwa kuripoti Agosti kwenye makambi ya JKT waliyopangiwa.\r\n\r\n\"Kwa upande wa vijana wa mujibu wa sheria, JKT limetoa orodha ya awamu ya pili ya majina ya vijana waliohitimu elimu ya kidato cha sita 2019 kwa ajili ya kujiunga na mafunzo,\" ilielezwa katika taarifa hiyo.\r\n\r\nMkuu huyo wa JKT amewaeleza kuwa katika mafunzo hao vijana watapata fursa ya kujifunza uzalendo, ukakamavu, stadi za kazi na maisha zitakazowasaidia kujiajiri baada ya kuhitimu mafunzo hayo.\r\n\r\nAwali mwishoni mwa Mei JKT, ilitangaza majina ya vijana waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita kwa mwaka 2019 iliyowachagua, kutoka shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria.\r\n\r\nJehi hilo lilitangaza makambi watakayokwenda kupatiwa mafunzo hayo kwa muda wa miezi mitatu na wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 01 hadi 07 Juni 2019.\r\n\r\nKambi za JKT walizopangiwa vijana hao ni pamoja na Rwamkoma-Mara, JKT Msange-Tabora, JKT Ruvu-Pwani, JKT Mpwapwa na JKT Makutupora-Dodoma.\r\n\r\nNyingine ni JKT Mafinga-Iringa, JKT Mlale-Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba-Tanga, JKT Makuyuni-Arusha, JKT Bulombora, JKT Kanembwa, na JKT Mtabila –Kigoma, JKT Itaka-Songwe, JKT Lua na JKT Milundikwa-Rukwa, JKT Nachingwea-Lindi.