Ndugai awashangaa wabunge kuwekeza kwenye Bodaboda na Noah badala ya elimu

Campus Admin 2019-06-11 17:30:53 Campus News

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai, ametoa wito kwa wabunge kuwekeza kwenye sekta ya elimu badala ya magari aina ya Noah au pikipiki, akieleza kuwa wanamtia aibu.\r\n\r\nNdugai alitoa kauli hiyo jana bungeni jana alipokuwa akitangaza wageni wa Mbunge wa Bukoba Vijijini, Jasson Rweikiza (CCM), ambao ni wanafunzi waliofanya vizuri kidato cha nne na darasa la saba mwaka 2018.\r\n\r\nWanafunzi waliotambulishwa ni waliomaliza kidato cha nne mwaka 2018 katika Shule ya Sekondari Sunshine na kupata ufaulu wa daraja la kwanza na pili.\r\n\r\n\"Pia kuna wanafunzi 59 waliomaliza darasa la saba mwaka 2018 kutoka Shule ya Msingi ya Anne Marie Academy ya jijini Dar es Salaam, kwenye wilaya, hii shule ya ilikuwa ya kwanza na kimkoa ilikuwa ya kwanza na kitaifa ilikuwa ya sita,\" alisema.\r\n\r\nKutokana na ufaulu huyo, Spika Ndugai alimpongeza Rweikiza ambaye ni mmiliki wa Shule ya Anne Marie kwa kuimarisha elimu.\r\n\r\n\"Haya ndo mambo ambayo wabunge tunatakiwa tufanye, siyo mbunge unamiliki Noah, unamtia aibu Spika, kila siku unaonekana trafiki huko, mbunge unamiliki bodaboda!\r\n\r\n\"Tuvuke jamani, bodaboda zikikamatwa, unampigia Spika, Spika bodaboda zangu zimekamatwa huku,\" Ndugai alisema na kuibua vicheko bungeni.\r\n\r\nKiongozi huyo wa Bunge alitoa rai kwa watunga sheria hao kuwekeza kwenye mambo makubwa, akisema wanapaswa \"kuvuka kidogo kwenye uwekezaji\".\r\n\r\nNje ya Ukumbi wa Bunge, Mkuu wa Shule ya Msingi, St. Anne Marie, Gladius Ndyetabura, alisema wanafunzi 59 wa shule hiyo waliofanya mtihani wa kumaliza darasa la saba mwaka jana, walipata wastani wa alama A na kuiwezesha kushika nafasi ya sita kitaifa na ya kwanza Mkoa wa Dar es Salaam.\r\n\r\n\r\nNdyetabura alisema imekuwa kawaida kwa shule hiyo kuwapa motisha wanafunzi wa shule hizo na ndiyo sababu shule imekuwa ikipata matokeo mazuri kwenye mitihani mbalimbali ya kitaifa.\r\n\r\nAlisema mbali na kufanya ziara bungeni, wanatarajia kuanza kuwapeleka Dubai, Uingereza na Marekani wanafunzi watakaokuwa wanafanya vizuri kwenye mitihani yao ili iwe chachu kwa wengine kufanya vyema zaidi.\r\n\r\n\"Shule imejiwekea utaratibu wa kuwapa motisha wanafunzi wanaofanya vizuri zaidi na huwa tuna kawaida ya kuwapeleka mbuga za wanyama kama Serengeti, Mikumi, Ngorongoro... tutaanza kuwapeleka Ulaya,\" alisema.