Mwanafunzi aua mwenzake kwa kumpiga jiwe kisogoni

Campus Admin 2019-06-11 17:59:02 Campus News

\r\nHabari na Hoja mchanganyiko\r\nMwanafunzi aua mwenzake kwa kumpiga jiwe kisogoni\r\n T miss zomboko S Today at 2:22 PM\r\nJUMP TO NEW\r\nWATCH\r\nMiss Zomboko\r\nJF-Expert Member\r\nToday at 2:22 PM\r\nNew\r\nA\r\n#1\r\n\r\nMtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Rashid Said (17) amefariki dunia baada ya kudaiwa kupigwa jiwe lililompata kichwani eneo la kisogoni na mwenzake ambae ni mwanafunzi wa shule ya sekondari Nyumbu huko Kibaha mkoani Pwani.\r\n\r\nKamanda wa Polisi mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa amesema kuwa tayari jeshi la Polisi linamshikilia mwanafunzi huyo ili kuendelea na taratibu za kisheria.\r\n\r\nAlieleza kuwa Juni 7 mwaka huu maeneo ya Pichandege marehemu alijeruhiwa kwa kupigwa jiwe baada ya tukio hilo alipelekwa katika hospital ya rufaa ya Tumbi kwa matibabu ambapo siku iliyofuata alifariki dunia.\r\n\r\nMwili wa marehemu umepelekwa hospital ya taifa ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi. \r\n\r\nJeshi la polisi Pwani limetoa wito kwa jamii kuacha kujichukulia sheria mkononi ili kujiepusha na matatizo ama kujikuta wakichukuliwa hatua za kisheria.